Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:01

Mapigano yazuka tena nchini Sudan licha ya ahadi ya sitisho la mapambano


Vifusi vya nyumba iliyoshambuliwa katika mapigano ya hivi karibuni mjini Khartoum, Aprili 25, 2023.
Vifusi vya nyumba iliyoshambuliwa katika mapigano ya hivi karibuni mjini Khartoum, Aprili 25, 2023.

Mapigano yalipamba moto tena nchini Sudan Jumanne licha ya pande zinazozozana kutangaza sitisho la mapigano, huku watu zaidi wakiuhama mji wa Khartoum na maafisa wa zamani wa serikali, akiwemo mmoja anayekabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita wa kimataifa wakitoroka jela.

Jeshi la Sudan na wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) walikubaliana kusitisha mapigano kwa saa 72 kuanzia jana Jumanne baada ya mazungumzo yaliyofanyika chini ya upatanishi wa Marekani na Saudi Arabia.

Lakini milio ya risasi na milipuko ilisikika katika mji wa Omdurman baada ya usiku kuingia, moja ya mji pacha wa Khartoum kwenye mto Nile ambako jeshi lilitumia ndege zisizo na rubani (drones) kulenga maeneo ya RSF, mwandishi wa habari wa Reuters amesema.

Jeshi lilitumia pia droni kujaribu kuwarudisha nyuma wapiganaji kutoka kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta kwenye makutano ya Blue Nile na White Nile.

Tangu mapigano kuzuka kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF tarehe 15 Aprili, na kukwamisha mchakato wa kurejesha utawala wa kidemokrasia wa kiraia, wanamgambo wamejikita katika maeneo ya makazi na jeshi linajaribu kuwalenga kwa mashambulizi ya anga.

Mapigano yamegeuza maeneo ya makazi kuwa uwanja wa mapambano. Mashambulizi ya anga na mizinga yameua takriban watu 459, kujeruhi wengine zaidi ya 4,000, kuharibu hospitali na kupunguza usambazaji wa chakula katika taifa ambalo tayari linategemea msaada kwa theluthi moja ya raia wake milioni 46.

XS
SM
MD
LG