Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:40

Juhudi za kusitisha mapigano Sudan zazaa matunda


Mkuu wa jeshi la Sudan, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na kiongozi wa Vikosi vya Rapid Support Forces (RSF), Mohamed Hamdan Daglo (Kulia). Picha na Akuot Chol na Ashraf SHAZLY / AFP.
Mkuu wa jeshi la Sudan, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na kiongozi wa Vikosi vya Rapid Support Forces (RSF), Mohamed Hamdan Daglo (Kulia). Picha na Akuot Chol na Ashraf SHAZLY / AFP.

Makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani ya kusitisha mapigano ya siku tatu kati ya majenerali wanaopigana Sudan yanaonekana kuzaa matunda, licha ya mapigano ya hapa na pale,baada ya juhudi za awali za kusitisha mapigano kushindikana.

Watu katika mji mkuu wanaitumia hali ya utulivu uliopo katika mapigano ili kukusanya tena mahitaji muhimu au kulihama jiji la Khartoum.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken Jumatatu alitangaza kwamba pande zinazo zozana nchini Sudan zimekubaliana kusitisha mapigano kwa saa 72.

Blinken alisema makubaliano kati jeshi la Sudan (SAF) au SAF, na Rapid Support Forces (RSF), yalianza "kufuatia mashauriano mazito katika muda wa saa 48 zilizopita."

"Marekani imeyataka majeshi ya SAF na RSF kuunga mkono mara moja na kikamilifu usitishaji mapigano," Blinken alisema.

Alisema Marekani itashirikiana na washirika wa kikanda na wa kimataifa na wadau wa kiraia wa Sudan kusaidia kuunda kamati yenye lengo la kupatikana kwa "sitisho la kudumu la mapigano na kuweka mipango ya masuala ya kibinadamu nchini Sudan."

Katika taarifa ya maandishi ya Jumatatu, RSF ilisema imekubali kusitisha mapigano "ili kufungua njia za kibinadamu, kuwawezesha raia na wakaazi kutoka na kwenda kujipatia mahitaji yao muhimu, kwenda hospitali na maeneo salama na kuwezesha balozi kuwaondoa wafanyakazi wao."

"Pia tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati na kuweka shinikizo kwa jeshi la Sudan kutii masharti ya kusitisha mapigano," ilisema RSF kupitia mtandao wa Twitter.

Hakuna taarifa rasmi za haraka kutoka kwa jeshi la Sudan kuhusu usitishaji mapigano uliosimamiwa na Marekani.

Siku ya Jumanne raia wa mji wa Khartoum walijitosa kununua chakula na mahitaji muhimu siku ya au walipakia kwenye magari kuutoroka mji huo, wakitafuta maeneo salama wakati kusubiri mapigano hayo, ambayo yalianza Aprili 15.

Kuwaondoa wanadiplomasia kutoka Khartoum kuliendelea kwa siku ya tatu.

XS
SM
MD
LG