Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:27

Hofu imetanda Sudan kwa simba takribani 25 na wanyama wengine kukosa chakula


Mfano wa Simba ambao wanaelezewa kukosa chakula nchini Sudan kutokana na mapigano yanayoongezeka huko. (US National Park Service, via AP)
Mfano wa Simba ambao wanaelezewa kukosa chakula nchini Sudan kutokana na mapigano yanayoongezeka huko. (US National Park Service, via AP)

Kituo kinachohifadhi wanyamapori kimesema hakina umeme kwenye uzio kwasababu ya usalama kuzunguka maeneo yake na kwamba kinapungukiwa chakula kwa ajili ya simba ambao kila mmoja anahitaji kilo tano hadi 10 za nyama kwa siku.

Mapigano makali nchini Sudan ambayo yamelitumbukiza taifa hilo katika vurugu na kuuliwa kwa mamia ya watu pia yameongeza hofu kuhusu hatma ya simba 25 na wanyama wengine katika hifadhi ya wanyamapori.

Kituo hicho kimesema hakina umeme katika uzio kwasababu ya usalama kuzunguka eneo hilo na pia kinapungukiwa na chakula kwa ajili ya simba hao, ambao kila mmoja anahitaji kilo tano hadi 10 za nyama kwa siku.

Ghasia zilizuka katika mji mkuu na kote Sudan hapo Aprili 15 kati ya vikosi vinavyomtii mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake aliyegeuka hasimu wake Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza vikosi vya Rapid Support Forces.

Mapigano hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400 na kuwajeruhi maelfu ya watu pamoja na kutishia kuingia katika kiwango kikubwa cha machafuko katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika ambayo tayari ni moja ya nchi maskini sana duniani.

XS
SM
MD
LG