Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:10

Mapigano bado yanaendelea Sudan


Moshi unaonekana kutanda katika mji wa Khartoum nchini Sudan. April 22, 2023.
Moshi unaonekana kutanda katika mji wa Khartoum nchini Sudan. April 22, 2023.

Baadhi ya uhamishaji  unafanyika kutoka Port Sudan kwenda Bahari ya Sham mwendo wa umbali wa  kilomita 850 kwa njia ya barabara kutoka Khartoum. 

Mapigano yanayoendelea nchini Sudan yameibua operesheni kadhaa za kuwahamisha raia wa kigeni au wafanyakazi wa ubalozi kwa njia ya barabara, anga na bahari.

Uwanja mkuu wa ndege katika mji mkuu Khartoum umekuwa eneo la mapigano makali na uko chini ya udhibiti wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) ambavyo vinapambana na jeshi. Baadhi ya uhamishaji unafanyika kutoka Port Sudan kwenda Bahari ya Sham mwendo wa umbali wa kilomita 850 kwa njia ya barabara kutoka Khartoum.

XS
SM
MD
LG