Mvutano wa kisiasa umezidi kuongezeka Drc kabla ya upigaji kura wa desemba 20 ambapo rais Felix Tshisekedi anatarajia kuwania tena muhula wa pili.
Vikosi vya usalama vilifyatua gesi ya kutoa machozi katika maandamano ya kuipinga serikali mwishoni mwa wiki huku waandamanaji wakirejea malalamiko ya wagombea wa upinzani juu ya uchelewesho na hitilafu katika maandalizi ya kuelekea upigaji kura.
Waandamanaji katika taifa hilo lenye watu takriban milioni 95 pia walikasirishwa na kupanda kwa gharama za maisha na ongezeko la ghasia upande wa mashariki , ambako makundi ya wanamgambo yenye silaha wanagombea ardhi na rasilimali za madini.
Ukosefu wa usalama umepelekea ugumu wa kujiandikisha wapiga kura katika maeneo kadhaa . CENI imesema inatafuta suluhisho ili kuwaandikisha.