Tume ya mpito ya amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia inatarajia kupata kiongozi mpya katika siku zijazo baada ya uhusiano kati ya serikali iliyowapokea na mkuu wa tume ya ulinzi kuharibika wiki iliyopita.
Vyanzo vya kidiplomasia vimeliambia gazeti la The East African itakuwa ni “muhali” kwa Francisco Madeira kurejea Somalia baada ya nchi hiyo kumuondolea hadhi ya kidiplomasia.
Chanzo kilisema Bwana Madeira, raia wa Msumbiji, alikuwa anashinikizwa kujiuzulu ili isionekane kwamba alikuwa amefukuzwa kazi.
Bw Madeira alikuwa hajajibu maswali yetu.
Mkuu wa Tume ya mpito ya amani ya Umoja wa Afrika (Atmis) angelikuwa anasherehekea wiki chache za awali za chombo hicho kipya cha kulinda amani, baada ya Amisom, sehemu kubwa ni tume ya kijeshi iliyokuwa ikiwalenga al-Shabaab iliyodumu kwa miaka 13, imebadilishwa kwa kuletwa nyingine.
Kipindi cha mpito, hata hivyo, kimeenda sambamba na taarifa zilizotolewa kuwa Madeira aliingia katika matatizo na serikali ya Somalia baada ya sauti yake ilipobainika ikiwakashifu maafisa wa serikali kwa udhaifu wao wa kushughulikia matatizo ya usalama.
Kuanzia Alhamisi wiki hii Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat alikuwa akionyesha kusita waziwazi kuwa “ana imani kamili” na Bw Madeira, msimamo ulioungwa mkono na Rais wa Somalia Mohamed Farmaajo , lakini wakati Waziri mkuu wake Hassan Roble hakubaliani naye..
Siku ya Jumatatu, Bw Roble alitekeleza amri ya kufukuzwa Bw Madeira, ikiwemo kumoundolea hadhi ya kidiplomasia kama kutumia ukumbi wa VIP kwenye uwanja wa ndege, kufuta kibali chake cha kazi cha kidiplomasia na hadhi nyingine alizokuwa nazo wakati akihudumu kama mwakilishi maalum wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika na mkuu wa Atmis.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African