Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:56

Kinyang'anyiro cha nafasi ya uongozi Jumuiya ya Madola ni jaribio kwa Rwanda


FILE -Rais wa Rwanda Paul Kagame
FILE -Rais wa Rwanda Paul Kagame

Kuingia Jamaica katika kinyang’anyiro cha nafasi ya juu kwenye Jumuiya ya Madola kunaweza kuwa ni maumivu ya kidiplomasia kwa Rwanda wakati Kigali ikijitayarisha kuwa mwenyeji wa mkusanyiko wa nchi wanachama 54 wa jumuiya hiyo huku wakiwa hawajakubaliana nani ni mgombea wao wote.

Aprili 1, Jamaica ilitangaza kuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Kamina Johnson Smith, atagombea nafasi hiyo ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.

Kamina Johnson Smith (AP Photo/Bebeto Matthews)
Kamina Johnson Smith (AP Photo/Bebeto Matthews)

Tangazo hilo limewagawa wanachama wa umoja wa nchi za Caribbean (Caricom), ambao awali walikuwa wanamuunga mkono Katibu Mkuu wa sasa, Baroness Patricia Scotland, ambaye anawania kipindi cha pili.

Akiungwa mkono na Dominica, ambako alizaliwa na mama raia wa Dominica and baba raia wa Antigua, Bi Scotland alishinda mara iliyopita baada ya pande zote za eneo la Afrika na Caribbean kumuunga mkono

Uingereza, ambako alikulia, haikuunga mkono kuchaguliwa kwake 2015. Pia haijaahidi kufanya hivyo mara hii pia.

Wakati nchi zenye ushawishi katika jumuiya hiyo – Uingereza, Canada, New Zealand na Australia hawajamuidhinisha hadharani mgombea yoyote, vyanzo vya ndani ya jumuiya vimeliambia gazeti la The East African kuwa kuna uwezekano wakamuunga mkono mgombea wa Jamaica kwani Johnson Smith anaheshimiwa nchini kwake na nje ya nchi.

Bi Scotland amekuwa chini ya uchunguzi na wanachama wa nchi tajiri baada ya ukaguzi wa ndani wa 2020 kubaini kuwa alitoa mkataba mnono kwa rafiki yake.

Alikanusha shutuma hizo na alisisitiza kuwa alifuata kanuni za manunuzi za jumuiya hiyo.

Janga la COVID-19 lilivyoingilia kati

Mkutano wa Jumuiya ya Madola wa Viongozi wa Serikali (Chogm) ulitakiwa kufanyika mwezi Juni 2020 lakini uliahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa COVID-19.

Kufuatana na mkutano wa mwaka huu, Bi Scotland angekuwa ametumikia miaka miwili zaidi katika kipindi chake cha kwanza.

Awali alikabiliwa na ushindani kutoka kwa mgombea wa Kenya Monica Juma, ambaye ni Waziri wa Ugatuzi . Lakini Machi, Dr Juma alijitoa katika kinyang’anyiro hicho, akieleza kushindwa kwake kuzishawishi nchi za Caribbean kumuunga mkono.

Monica Juma
Monica Juma

Chini ya mfumo wa upigaji kura katika Jumuiya ya Madola ambao unatoa kipaumbele cha makubaliano, wanachama wote lazima wakubaliane juu ya mgombea au hawezi kutangazwa mshindi.

Maafisa wa Rwanda hawakutoa maelezo mara moja juu ya suala hilo.

Kwa upande wa Kigali hilo wanalitaka ili kufanikisha mkutano wa CHOGM, kinyang’anyiro ambacho tayari kimeyagawa mataifa ya Carribean pakubwa, na inaleta pingamizi jingine la kidiplomasia mbele ya mkutano huo wa Juni 2022.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African, Kenya

XS
SM
MD
LG