Tshisekedi mwenye umri wa miaka 55, mtoto wa marehemu Icon Etienne aliyekuwa ni muasisi wa upinzani, aliapishwa kushika madaraka katika Kasri ya Wananchi, ambako liko Bunge la taifa katika mji mkuu wa Kinshasa.
Wafuasi wake ambao kwa miongo kadhaa walimuunga mkono Tshisekedi katika kutafuta madaraka walijitokeza katika mtaa huo wakiwa na bendera zilizo kuwa zimepachikwa kwenye nywele zao au wakiwa wamevaa kofia zenye picha ya chui.
Wakongo wengi wanamatumaini kuwa Tshisekedi ataleta mabadiliko baada ya miaka 18 ya utawala wa Rais Joseph Kabila, ambaye katika hotuba yake ya mwisho Jumatano usiku alihimiza nchi iungane katika kumuunga mkono kiongozi huyo.
Alisema kuwa anaachia madaraka bila masikitiko yoyote.
Hata hivyo Tshisekedi ni lazima afanye kazi na bunge ambalo lina wabunge walio wengi wa chama tawala cha Kabila.