Akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu maafisa wa wizara ya ulinzi kuthibitisha kuwa shambulizi la anga karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad Ijumaa lilikuwa limekusudia kumuua Soleimani. Trump ameionya Iran kuwa inajiweka hatarini kwa kukabiliwa na mashambulizi zaidi iwapo itaendelea kuwalenga Wamarekani.
“Tumechukua hatua usiku wa jana kuzuia vita, “Trump amewaambia waandishi wa habari akiwa nyumbani kwake Mar-a-Lago, Florida.
“Hata hivyo, vitendo vya uchokozi vinavyo fanywa na serikali ya Iran katika eneo, ikiwemo kutumia wapiganaji walioko katika eneo kuyumbisha majirani zao, ni lazima ukome, na lazima ukome hivi sasa.
Trump alimlaumu Soleimani kwa kusababisha vifo vya maelfu ya Wamarekani, Wairaqi na Wairan, akisema jenerali huyo aliyetumikia kwa muda mrefu “ alifanya vifo vya watu wasiokuwa na hatia ni maradhi ya utashi wake” wakati akisaidia kuendesha mitandao ya kigaidi ambayo imeenea Mashariki ya Kati hadi Ulaya na Marekani.
“Tunapata faraja kujua kuwa usimamizi wake wa kigaidi umemalizika,” rais alisema, akiongeza kuwa Marekani tayari imeshatambua maeneo mengine kadhaa ya kuyashambulia.
Maafisa wa Iraqi wamesema kuwa shambulizi jingine la anga lilifanyika mapema Jumamosi, baada ya masaa 24 ya lile lililomuua Soleimani, yaliwalenga msafara wa wanamgambo wanaosaidiwa na Iran Kaskazini mwa Baghdad na kuua watu wasiopungua watano. Hakuna habari za kuthibitisha shambulio hilo zilipatikana mara moja kutoka Washington.