Trump ajadili nyaraka za siri za kiwango cha juu katika mahojiano yaliyorikodiwa na mwandishi

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Sauti iliyorikodiwa ambayo iko mikononi mwa vyombo vya habari inabainisha  Rais wa Marekani Donald Trump akijadili nyaraka za siri kuhusu mpango wa kuishambulia Iran wakati akizungumza na mwandishi baada ya kuondoka madarakani mwaka 2021.

Iran

Waendesha mashtaka wa serikali kuu wameeleza sehemu ya mazungumzo hayo katika mashtaka yaliyofunguliwa mwezi uliopita kuwa alikuwa anashikilia kinyume cha sheria nyaraka za siri za serikali na baadae alifanya njama ya kuzuia uchunguzi wa serikali kuu.

Kituo cha televisheni cha CNN, gazeti la The Washington Post na gazeti la New York Times walitoa rekodi ya sauti siku ya Jumatatu ambapo Trump anazungumzia ripoti kuwa Mwenyekiti wa wakuu wa Majeshi Jenerali Mark Milley alihofia kuwa Trump anaweza kutengeneza vita dhidi ya Iran baada ya kushindwa uchaguzi wa rais mwaka 2020.

Jen. Mark Milley

“Kuhusu Milley, wacha niangalie, nitakuonyesha mfano,” Trump anasema katika rekodi hiyo, ambayo inajumuisha sauti ya mlio wa makaratasi.

“Alisema kuwa ninataka kuishambulia Iran. Je, hilo si linashangaza? Nina mlima wa nyaraka; hili jambo limejitokeza. Angalia, hii ilikuwa ni yeye, waliniletea mimi hiki. Hili, halitakiwi kusajiliwa, lakini walinipa hiki, Hii ilikuwa ni yeye. Hii ilikuwa wizara ya Ulinzi na yeye.”

“Hii inanipa ushindi kwa kesi yangu, wewe unafahamu? Trump alisema. “Isipokuwa tu, ni siri ya hali ya juu, siri. Hii ni taarifa ya siri.

Trump baadae alisema, “Unaona, kama rais ningeweza kuifanya isiwe siri tena, hivi sasa siwezi tena.”

Rais huyo wa zamani alisema yeye alikuwa na ruhusa kufuta usiri wa nyaraka hizo zote zilizochukuliwa kutoka ofisi ya Oval hadi makazi ya White House. Alikana mashtaka alipofika mahakamani Juni.