Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 00:13

Trump afika mbele ya hakimu mjini Miami, akanusha mashtaka katika kesi ya kihistoria


Rais wa Zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa Zamani wa Marekani Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Jumanne alasiri alifika mbele ya hakimu wa mahakama ya serikali kuu mjini Miami, Florida, amekanusha mashtaka ya kuhifadhi kinyume cha sheria mamia ya nyaraka za siri za serikali baada ya kuondoka Ikulu, na kuzuia juhudi za serikali kuzipata.

Trump aliweka historia wiki iliyopita wakati jopo la mahakama lilipomshtaki kwa makosa 37 ya uhalifu, yakiwemo makosa 31 ya "kuhifadhi kwa makusudi" taarifa za siri za ulinzi wa taifa, huko Mar-a-Lago, katika makazi yake kwenye jimbo la Florida.

Kushtakiwa kwa rais huyo wa zamani kulifanyika chini ya ulinzi mkali, huku mamia ya wafuasi wa Trump walikusanyika nje ya mahakama.

VOA Swahili imezungumza na mchambuzi wa siasa za Marekani Prof. David Monda ambaye ambaye anaanza kwa kuelezea umuhimu wa kesi hii iliyogonga vichwa vya habari kitaifa na kimataifa.

Mazungumzo ya mchambuzi wa siasa David Monda na VOA Swahili.m4a
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:21 0:00

Trump alikuwa ametoa wito kwa wafuasi wake kuandamana huko Miami, akizua wasiwasi kwamba mkusanyiko huo ungeweza kugeuka kuwa ghasia. Lakini mchakato huo haukuwa na matukio yoyote makubwa.

Forum

XS
SM
MD
LG