UNESCO ilisema katika taarifa yake kwamba hatua hiyo inashirikisha “mpango kamili wa ufadhili” ambao lazima upitishwe na nchi wanachama.
Kabla ya kujiondoa, Marekani ilikuwa ni mfadhili mkuu wa UNESCO, ikitoa takriban asilimia 22 ya bajeti ya shirika hilo.
Lakini ilisitisha michango ya kifedha mwaka 2011 baada ya uanachama wa Palestina kupitishwa na kujiondoa kabisa mwaka 2018 wakati wa uongozi wa Trump ulipoituhumu UNESCO kuwa inaegemea upande mmoja dhidi ya Israeli.
UNESCO ilisema katika miaka ya hivi karibuni imefanya kazi kupunguza mvutano wa kisiasa na kufikia mwaafaka katika maudhui nyeti, kama vile suala la Mashariki ya Kati.
“Hii ni hatua muhimu ya kuongeza imani kwa UNESCO na ushirikiano wa kimataifa,” Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Azoulay alisema katika taarifa yake.
“Siyo tu idhini ya taasisi hiyo kusimamia – utamaduni, elimu, sayansi na taarifa – lakini pia katika namna ya mamlaka yake yanavyotekelezwa kila siku.”
Rais wa Marekani Joe Biden ameomba dola za Marekani milioni 150 kutolewa kwa UNESCO katika bajeti ya mwaka 2024 na kulipa michango yake ya miaka ya nyuma.
Maafisa wa Marekani walisema kabla ya tangazo hilo Jumatatu kuwa kutokuwepo katika UNESCO inaipatia nguvu China katika masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na katika suala la kuweka viwango vya Artificial Intelligence.
Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP na AFP.
Forum