Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:25

China yakanusha madai ya Marekani inafanya ujasusi Cuba


Antony Blinken
Antony Blinken

China Jumatatu imekanusha madai ya Marekani kuwa inaendesha kituo cha ujasusi nchini Cuba.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Wenbin alisema katika mkutano wa waandishi wa habari kuwa madai hayo yalikuwa ya uongo na kwamba Marekani ilikuwa inatoa taarifa zinazokinzana.

Maelezo ya Wang yametolewa siku kadhaa baada ya maafisa wa utawala wa Biden kusema China ilikuwa inaendesha operesheni za kijasusi huko Cuba, ambayo iko kilomita 200 kutoka jimbo la Marekani la Florida, kwa muda sasa.

Katika ujumbe wa Twitter Jumamosi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Carlos Fernandez de Cossio aliyaita madai hayo “uvumi mbaya wa kuharibu sifa.”

Matokeo hayo yanajiri wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa kufanya ziara mjini Beijing hivi karibuni.

Mipango yake ya awali kuhusu kwenda China Februari ilisitishwa wakati mvutano ulizuka kati ya nchi hizi mbili wakati puto la kijasusi la China lilipokwa katika anga ya Marekani.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG