Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 00:12

Rais wa zamani Marekani Donald Trump amefunguliwa mashtaka


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump. April 14, 2023.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump. April 14, 2023.

Trump alithibitish habari hizo kwenye ukurasa wa mtandao wake wa True Social kwamba mawakili wake walimuarifu kwamba wizara ya sheria imemfungulia mashtaka na kwamba ametakiwa kujiwasilisha mbele ya mahakama mjini Miami siku ya Jumanne

Vyombo kadhaa vya habari vya Marekani vinaripoti kwamba Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amefunguliwa mashtaka kutokana na jinsi alivyoshughulikia waraka za siri za serikali baada ya kuondoka White House. kwa madai ya kutumia vibaya nyaraka nyeti za serikali.

Trump alithibitish habari hizo kwenye ukurasa wa mtandao wake wa True Social kwamba mawakili wake walimuarifu kwamba wizara ya sheria imemfungulia mashtaka na kwamba ametakiwa kujiwasilisha mbele ya mahakama mjini Miami siku ya Jumanne.

Mashtaka hayajafunguliwa lakini shirika la habari la CNN inawanukua baadhi ya maafisa wanaofahamu kesi hiyo kwamba amefunguliwa mashtaka kadhaa ya uhalifu. Hatua hiyo inamfanya Trump kua rais wa kwanza wa zamani kushtakiwa na mahakama ya serikali kuu.

Mawakili wa Trump hawakujibu mara moja ombi la kutoa maoni kuhusiana na taarifa hiyo. Msemaji wa mwanasheria maalum Jack Smith, ambaye anashughulikia uchunguzi huo, alikataa kutoa maoni yake.

Forum

XS
SM
MD
LG