Ziara itaangaza fursa za kupiga picha kuliko kufanya makubaliano inaweza kuwa ni jambo la kusudi lililoandaliwa na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, ambaye amejenga uhusiano wa karibu na Trump. Wawili hao wamekutana au kuzungumza zaidi ya mara 40, kitu ambacho hakijawahi kutokea kabisa na viongozi wengine,” kwa mujibu wa White House.
Profesa katika Chuo Kikuu cha Keio Tomohiko Taniguchi, mwandishi mkuu wa hotuba za waziri mkuu zinazohusu sera za kigeni, anafikiria kuwa mbali na upande wa tafrija wa ziara hiyo, kutakuwa na mambo machache muhimu yatakayo jitokeza.
Lakini Taniguchi anaeleza kuwa Abe ni kiongozi pekee wa kigeni ambaye “Trump anaweza kutumia masaa kadhaa wa kadhaa bila ya kuandaa nukta za mazungumzo yake, na hicho kinafanya kuwepo mkakati wenye thamani kwa diplomasia ya Japan.
Alipoulizwa na VOA iwapo ziara hiyo itakuwa na tija ya kuwepo matokeo ya ushirikiano wa kibiashara na ulinzi, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani akieleza juu ya ratiba ya Trump na Abe ya Jumatatu juu ya kufanyika kwa mkutano na waandishi wa habari, “ watakuwa na matangazo yenye kuvutia sana juu ya kiwango cha mahusiano yao.”