Tathmini ya Uingereza yaonyesha Russia ilishambuliwa kutokana na jeshi lao kuwa halina weledi

Athari za shambulizi la majeshi ya Ukraine dhidi ya majeshi ya uvamizi ya Russia yaliyoko Ukriane.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumatano kwamba  shambulizi la Ukraine kwenye  kambi ya jeshi katika eneo mji  unaodhibitiwa na Russia ulioko mashariki mwa inawezekana umechangiwa  zaidi na  Russia kuhifadhi silaha karibu na wanajeshi wa Russia wanakoishi.

“Kutokana na kiwango cha uharibifu, kuna ukweli wa uwezekano kwamba silaha zilikuwa zimehifadhiwa karibu na makazi ya wanajeshi, ambazo zililipuka wakati wa shambulizi hilo , na na hivyo kuteguka wakati wa shambulizi,” wizara hiyo iliandika katika Twitter ikiwa ni tathmini yake ya karibuni ya kila siku.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imeongeza kwamba Russia ilikuwa na historia ya uhifadhi usio salama wa silaha kabla ya kuanzisha uvamizi wake kwa Ukraine, “lakini tukio hili linaonyesha jinsi ukosefu wa weledi unavyochangia kiwango cha juu cha vifo kwa Russia.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema mapema Jumatano kwamba wanajeshi wake “wanatumia kwa wingi” simu za mkononi jambo ambalo lilipelekea shambulizi la Januari 1.

“Ni dhahiri kuwa sababu kuu kwa tukio hilo ni kuwasha na matumizi makubwa ya simu – kinyume na katazo – la wasimamizi wa simu za mkononi katika eneo linalofikiwa na silaha za adui,” wizara ilisema katika taarifa yake.

“Sababu hii iliruhusu adui kujua na kufuatilia uratibu wa mawasiliano ya wanajeshi hao eneo walipo ili kuwashambulia kwa makombora,” iliongeza.