Vituo hivyo vinahimiza kunusuru utawala wa sheria na kuheshimu itikadi mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa Alhamisi, ikiwa mara ya kwanza kwa maktaba hizi kuungana na kutoa tamko kwa umma, ilisema Wamarekani wanamaslahi muhimu katika kuunga mkono harakati za demokrasia na haki za binadamu ulimwenguni kwa sababu “jamii zilizo huru katika nchi nyingine zinachangia usalama wetu na mafanikio hapa nyumbani.”
“Lakini maslahi hayo,” ilisema taarifa hiyo, “yanapotoshwa wakati watu wengine wakiona nyumba yetu imekwenda mrama.”
Ujumbe huo wa pamoja kutoka vituo hivyo vya urais, taasisi zimehimiza umuhimu wa kuwa na utashi kwa wengine, uvumilivu na utofauti wakati ikiwasihi Wamarekani kuheshimu taasisi za kidemokrasia na kuendeleza uchaguzi salama na unaofikiwa na kila mmoja.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa “mdahalo na kutofautiana” ni msingi wa demokrasia lakini pia alitaja namna mdahalo ulivyoathirika katika safu za umma katika kipindi ambacho maafisa na familia zao wanapokea vitisho vya kuuawa.
“Ustaarabu na heshima katika majadiliano ya kisiasa, iwe katika mwaka wa uchaguzi au vinginevyo, ni muhimu,” imeeleza taarifa hiyo.
Wengi wa marais wa zamani ambao bado wako hai wamekuwa wakijitokeza kutoa maoni yao hadharani kuhusu hali ya taifa wakati utafiti wa maoni unaonyesha kuwa Warepublikan wengi bado wanaamini uongo unaoendelezwa na Rais wa zamani Donald Trump na washirika wake kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 ulikuwa umeibiwa.
Trump, Mrepublikan, pia ameshambulia mfumo wa mahakama wakati akikabiliwa na mashtaka katika kesi nne za uhalifu, ikiwemo mbili zinazohusiana na juhudi zake za kutaka kubadilisha matokeo ya uchaguzi ambao alishindwa na Joe Biden, Mdemokrat.
Taarifa ya Alhamisi ilisita kutaja majina ya watu binafsi, lakini bado ilionyesha ushahidi wa moja ya yale yanayoaminika kuwa watu wanaofungamana na marais wa zamani wa taifa hili wana wasiwasi kuhusu mustakbali wa nchi hii.
“Nafikiri kuna wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya demokrasia yetu wakati huu,” alisema Mark Updegrove, mkurugenzi mtendaji wa LBJ Foundation, ambayo inaisaidia Maktaba ya Rais ya LBJ huko Austin, Texas. “Hatuna haja ya kuingia ndani zaidi inatosha tukio la Januari 6 kutambua kuwa tuko katika hali ya hatari.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.