Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:06

Marekani yakumbuka tukio la uvamizi wa Bunge lililofanywa na genge la wafuasi wa Trump


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Ijumaa ni maadhimisho ya pili ya tukio la uvamizi wa Bunge la Marekani Januari 6, 2021, mjini Washington, wakati genge lenye hasira la wafuasi wa rais wa zamani Donald Trump likitaka kuzuia kurasmishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais ya 2020.

Kundi la wawakilishi wa pande zote katika Bunge watakusanyika upande wa ukumbi wa East Front Steps kwenye jengo la bunge Ijumaa asubuhi kuwaenzi maafisa waliopoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na uvamizi huo.

Rais wa Marekani Joe Biden anaadhimisha siku hiyo huko White House kwa sherehe ya kuwatunuku Medali ya Rais kwa Raia kwa watu 12, ambao afisa mmoja wa White House amesema, “ni michango yao iliyotukuka kulinda demokrasia ye kuhusiana na Januari 6, 2021.”

Medali hiyo ya Rais kwa Raia inawatambua raia wa Marekani kwa “utendaji uliotukuka wa kuitumikia nchi yao au raia wenzao.”

Kati ya watakao pokea tuzo hiyo Ijumaa ni mama na mtoto wake wa kike ambao walitishiwa kwa kufanya kazi yao kama wafanyakazi wa uchaguzi katika Kaunti ya Fulton, Georgia: maafisa wa polisi wa Bunge la Marekani na Washington D.C, wabunge, na mtumishi wa zamani wa serikali kuu.

Medali moja itatolewa kwa hayati Brian Sicknick, afisa wa polisi wa Bunge la Marekani, aliyepoteza maisha yake kwa kuwalinda maafisa waliochaguliwa. Alifariki Januari 7. Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris na familia zao walitoa heshima zao kwa Sicknick wakati mwili wake ulipowekwa kwa heshima zote katika ukumbi wa Bunge la Marekani wa Rotunda.

XS
SM
MD
LG