Sudan kutekeleza matakwa ya mataifa makubwa ili iondolewe vikwazo

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan

Serikali ya mpito ya Sudan inafikia makubaliano na mataifa makubwa juu ya masuala ya haki za binadamu ikiwa ni sehemu ya mpango kamili wa kuepukana na kutengwa kiuchumi.

Wiki iliyopita, maafisa mjini Khartoum wamesema watawakabidhi wananchi wa Sudan wote waliotuhumiwa na mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) inayotaka kusikiliza kesi zao huko The Hague.

Pia serikali hiyo inaendelea na mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kufidia familia za wanajeshi wa Marekani waliouawa katika shambulizi linaloihusisha Sudan, na hasa lile la tukio la Meli ya kivita ya Cole iliyoshambuliwa Yemen Octoba 2000.

Wakati huo, Wanamaji wa Marekani 17 waliuawa wakati magaidi walipodaiwa kulipua boti ndogo iliyokuwa karibu na meli hiyo ya Marekani iliyokuwa ikijaza Mafuta katika bandari ya Aden, limeripoti gazeti la The East African.

Taarifa hizi zimekuja kufuatia mkutano kati ya kiongozi wa Baraza huru la Mpito Abdel-Fattah al-Burhan na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu mjini Entebbe wiki mbili zilizopita. Mkutano huo ulikuwa unatafuta kufufua mahusiano kati yao ambayo yalikuwa yamekufa kwa miongo mitano.

Hili, na makubaliano mengine ambayo yanaweza kuonyesha Khartoum iko tayari kuchukua hatua na kufanya vikwazo vilivyowekwa dhidi yake kuondolewa.

Khalid al-Faki, mchambuzi wa siasa mjini Khartoum ameliambia gazeti la The East African kuwa serikali ya Waziri Mkuu Abdallah Hamdok inafanya kila inchoweza kuondolewa katika orodha ya nchi zilizowekewa vikwazo.

“Nafikiri kukubali kwa serikali ya Sudan na kukubali kwa waasi kuondolewa kwa rais Omar al-Bashir na watu wengine 52 wanaotuhumiwa na kukabidhiwa ICC kesi yao kusikilizwa kwa makosa ya jinai waliotenda huko Darfur ni shinikizo linalovuma,” amesema.