Maafisa wamesema Alhamisi waokoaji wanajaribu kuwafikia watu 21 waliokwama katika mafuriko kwenye machimbo haramu ya makaa kaskazini mwa China.
Mafuriko yalitokea Jumatano huko mjini Xiaoyi katika jimbo la Shanxi, kwa mujibu wa maafisa hao, kiasi cha kilometa 130 - kusini magharibi mwa mji mkuu wa jimbo Taiyuan.
Serikali ya Xiaoyi imesema katika mtandao wa kijamii kwamba maji yalikuwa yakitolewa kwa pampu kutoka kwenye machimbo hayo, na viwango vya maji vilikuwa vinapungua.
Kituo cha taifa cha utangazaji cha CCTV kimeonyesha picha za uokozi, na kusema waokozi hawajaweza kuwasiliana na watu 21 waliokwama kwenye machimbo hayo.
Polisi wamewatia mbaroni watu sita na wengine wanatafutwa kuhusiana na ajali hiyo, serikali imesema.