Shambulizi la Pittsburgh : Kile tunachokijua

Watu wakiomboleza vifo vilivyotokea baada ya shambulizi hilo kwa kuungana kuonyesha umoja wao na kufarijiana

Mkurugenzi wa Usalama wa Umma mjini Pittsburgh Wendell Hissrich amesema hali ndani ya Sinagogi la wahayudi ilikuwa yakusikitisha. "Moja kati ya shambulizi lililohuzunisha kuliko yote niliowahi kuyaona."

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (FBI) ikiendelea kuchunguza shambulizi hilo linalofungamana na chuki dhidi ya Wayahudi. Robert Bowers, 46, ambaye amefunguliwa mashtaka 11 ya jinai ya mauaji, makosa sita ya shambulizi lenyewe na 13 ya vitisho vya ubaguzi.

Vituo vya kukusanya damu huko Pittsburgh viliongeza masaa ya kuwahudumia watu waliokuwa wanataka kuchangia damu.

Miji ya New York na Los Angeles ziliimarisha usalama ikiwa ni tahadhari katika maeneo ya nyumba za ibada wakati taarifa ya mauaji hayo zilipoenea.

Rais Donald Trump amelaani shambulizi hilo, na kusema, “ Tukio hilo ovu, chuki iliyojaa sumu ya misimamo dhidi ya Wayahudi ni lazima ilaaniwe.”

Trump ameshauri kuwa Marekani lazima ifanye hima ya kuwepo sheria ya adhabu “Kali” kukabiliana na jinai kama hii.