Hakuna maelezo ya haraka kutoka kwa jeshi la Israeli, ambalo limekuwa likiendesha uvamizi karibu kila siku usiku katika majiji, miji na vijiji vilivyoko Ukingo wa Magharibi kwa kile inachosema ni jaribio la kuondoa harakati za wanamgambo.
Darzeni za Wapalestina wameuawa katika mashambulizi ya bunduki yaliyofanywa na Israeli mwaka huu na watu 19 wameuawa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na Wapalestina dhidi ya Waisraeli wakati huo.
Wizara ya Afya ya Palestina imemtambua kijana aliyeuawa kuwa ni Jibril al-Laada, aliyekuwa na miaka 17.
Imesema wengine watatu walijeruhiwa vibaya sana katika mapigano hayo, yaliyotokea katika kambi ya wakimbizi ya Aqabat Jabr karibu na mji wa Jericho, huko Ukingo wa Magharibi. Kambi hiyo imekuwa mara kwa mara inalengwa na uvamizi unaofanywa na Israeli.
Israeli imefanya uvamizi baada ya wimbi la mashambulizi ya Wapalestina majira ya mchepuko.
Hiyo ilichochea baadhi ya mashambulizi mabaya kati ya Israel na Wapalestina huko Ukingo wa Magharibi kwa miaka kadhaa wakati Israel ikisema uvamizi unakusudia kuzuia mashambulizi siku za usoni, ghasia dhidi ya Waisraeli hayaelekei kupungua.
Karibu Wapalestina 150 waliuawa huko Ukingo wa Magharibi na Jerusalem mashariki mwaka jana, ikiufanya mwaka 2022 kuwa ni mwaka wenye maafa makubwa katika maeneo hayo tangu mwaka 2004, kulingana na kikundi kinachoongoza kupigania haki za Waisraeli B’Tselem