Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:23

Papa Francis anaelezea wasiwasi wake kuhusu mivutano ya Israel na Wapalestina


Papa Francis kiongozi wa kanisa katoliki duniani akiwa katika misa ya Pasaka huko Vatican
Papa Francis kiongozi wa kanisa katoliki duniani akiwa katika misa ya Pasaka huko Vatican

Papa Francis alisema ghasia mpya zinatishia mazingira ya kuaminiana na kuheshimiana yanayohitajika ili kuanza tena mazungumzo kati ya wa Israeli na wa Palestina alisema wakati akihutubia umati wa maelfu ya watu waliokusanyika katika uwanja wa Saint Peter’s

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya kuzuka kwa mivutano kati ya Israel na Wapalestina wakati alipokuwa akiongoza misa ya Pasaka siku ya Jumapili.

Alisema ghasia hizo mpya zinatishia mazingira ya kuaminiana na kuheshimiana yanayohitajika ili kuanza tena mazungumzo kati ya Wa-israeli na Wa-palestina, alisema wakati akihutubia umati wa maelfu ya watu waliokusanyika katika uwanja wa Saint Peter’s.

Wiki hii imeshuhudia ongezeko la ghasia na machafuko wakati ambapo ni mwezi mtukufu wa Ramadan kwa Wa-islamu, Passover kwa Wayahudi, na Pasaka kwa wa-kristo vyote vikienda sambamba. Siku ya Jumatano, polisi wa Israeli waliuvamia ukumbi wa sala katika msikiti wa Al-Aqsa, eneo la tatu takatifu zaidi la wa-islamu katika uvamizi uliofanyika alfajiri uliolenga kuwaondoa vijana wanaovunja sheria na wachochezi waliokuwa wamejifunika nyuso zao ambapo walisema wamejifungia ndani ya msikiti huo.

XS
SM
MD
LG