Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:34
VOA Direct Packages

Wapiganaji wa Lebanon wadaiwa kurusha makombora Israel


Moshi kutokana na mashambulizi ya bomu kwenye mji wa Gaza City, Palestina, kwenye picha ya maktaba Feb. 23, 2023.
Moshi kutokana na mashambulizi ya bomu kwenye mji wa Gaza City, Palestina, kwenye picha ya maktaba Feb. 23, 2023.

Jeshi la Israeli limesema Alhamisi kwamba wapiganaji wa Lebanon wamerusha makombora mazito na kupelekea wakazi wa kaskazini mwa Israeli kukimbilia kwenye mahandaki ya kujikinga bomu.

Watu wawili wameripotiwa kujeruhiwa, na kuongeza hali ya taharuki, siku moja baada ya polisi wa taifa hiyo kufanya misako kwenye maeneo muhimu ya kidini mjini Jerusalem. Taarifa zimeongeza kusema kwamba roketi 34 zilirushwa ndani ya Israel, wakati 25 zikutunguliwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Iron Dome.

Idadi kubwa ya roketi zilozorushwa imeongeza hofu ya kuongezeka kwa mashambulizi wakati kundi adui la Israel linaloungwa mkono na Iran, Hezbollah, likiendelea kukita mizizi kwenye maeneo mengi kusini mwa Lebanon.

Katika siku mbili zilizopita, hali ya taharuki imeongezeka kwenye eneo takatifu la msikiti wa Al-Aqsa, mjini Jerusalem, pamoja na kwenye mpaka wa Israel wa Gaza. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameampa kwamba Israel itajibu vikali.

XS
SM
MD
LG