Serikali ya Afrika Kusini yatoa msaada wa dharura kufuatia mafuriko

Nyumba zilizosombwa na maji ya mafuriko katika eneo la Ntuzuma, nje ya mji wa Durban, Afrika Kusini, April 12, 2022, kufuatia mvua na mafuriko.

Serikali ya Afrika Kusini imetoa pesa kwa matumizi ya dharura, kuwasaidia maelfu ya watu walioachwa bila makazi, maji safi, na umeme.

Serikali ya Afrika Kusini imetoa pesa kwa matumizi ya dharura, kuwasaidia maelfu ya watu walioachwa bila makazi, maji safi, na umeme.

Hali hiyo imetokana na mafuriko yaliyoharibu maeneo yao na kuua takriban watu 400 pwani ya mashariki mwa nchi hiyo.

Mafuriko hayo katika jimbo la Kwazulu-Natal, yalisababisha umeme kukatika, na kuathiri shughuli katika bandari kubwa sana Afrika.

Waziri wa Fedha Enoch Godongwana, ameiambia televisheni ya serikali ya SABC kwamba dola milioni 68.3 zimetolewa kwa ajili ya kutoa misaada.

Pesa hizo zimetolewa baada ya jimbo la kwazulu-Nathal kutangazwa kuwa sehemu ya janga.

Maafisa wamesema kwamba uharibifu mkubwa sana umetokea kutokana na mafuriko hayo.

Shughuli za uokoaji zinaendelea.