Huku barabara na madaraja vikisombwa na mvua kubwa sana wiki hii, waokoaji walijitahidi kupeleka vifaa katika jiji lote, ambapo baadhi ya wakazi hawana umeme wala maji tangu Jumatatu.
“Kiwango cha uharibifu wa maisha ya watu, miundombinu, na mtandao wa utoaji wa huduma katika jimbo hilo haujawahi kutokea,” amesema Sihle Zikalala, mkuu wa Jimbo la KwaZulu Natal.
“Jumla ya watu 40,723 wameathirika. Cha kuskitisha ni kwamba, vifo 341 vimerekodiwa,” ameuambia mkutano wa waandishi wa habari.