Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Senegal Yassine Fall.
Aliongeza kuwa “Tuanasimamia hali ya eneo la Sahara na Sahel kuwa suala la makubaliano ya nchi za Afrika zenyewe.”
Misaada itakuwa zaidi kuimarisha ulinzi na kuboresha “kujiandaa kukabiliana na ugaidi wa vikosi vya kijeshi na huduma maalumu,” kulingana na Lavrov.
Pia amedai kuwa mazungumzo muhimu ya amani kati ya Russia na Ukraine “hayana umuhimu” baada ya Ukraine kuingia katika mkoa wa Kursk”
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Russia alisema,
“Rais wa Russia (Vladimir) Putin alikuja na mpango mwingine wa amani mwezi June, baada ya mipango yote ya amani iliyopita kuharibiwa na kuhujumiwa na utawala wa Kyiv na walezi wake wa Magharibi.”
“Kujitayarisha kwetu kwa mazungumzo kusingesababisha tatizo lolote na yoyote, ingawa, bila shaka, mazungumzo yeyote kuhusiana na suala hili yamekuwa hayana maana baada (ya Ukraine) kuingia katika mkoa wa Kursk, aliongeza.