Shirika la habari la Russia, Sputnik, lilimnukuu Zamir Kabulov, mjumbe maalum wa rais wa Afghanistan, akithibitisha makubaliano hayo saa chache baada ya mamlaka ya Taliban, kutoa maelezo ya makubaliano hayo.
Msemaji wa wizara ya biashara na viwanda wa Afghanistan, inayoongozwa na Taliban, Akhu-ndzada Abdul Salam, alisema maafisa wake wakuu walisafiri hadi mji mkuu wa Russia mwezi uliopita, ambako walijadiliana na kutia saini makubaliano hayo.
Mkataba huo utairuhusu Kabul kununua kila mwaka, tani milioni 1 za petroli, tani milioni 1 za dizeli, tani 500,000 za gesi ya kupikia, LPG, na tani milioni 2 za ngano kutoka Russia. Azizi alisema Moscow imewapunbguzia bei Taliban, na kwamba bidhaa hizo zitasafirishwa kwa barabara na reli.
Hata hivyo, hakufafanua kuhusu bei au mbinu za malipo.