Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 12:09

Taliban yatangaza Jumatatu kuwa siku kuu ya kitaifa


Askari wa Taliban wakiwa kwenye mji mkuu wa Kabul kwenye picha ya awali.
Askari wa Taliban wakiwa kwenye mji mkuu wa Kabul kwenye picha ya awali.

Utawala wa Taliban nchini Afghanistan umetangaza lJumatatu kuwa siku kuu ya kitaifa ya kuandhimisha mwaka mmoja tangu kuchukua tena madaraka kutoka kwa serikali iliyokuwa ikiungwa mkono kimataifa , wakati Marekani na NATO walipoondoa vikosi vyao nchini humo.

Taliban walishiks usukani kwa urahisi kwa kuwa hawakupata upinzani wowote kutoka kwa maafisa wa seriakli ya wakati huo, waliokuwa wamepewa mafunzo na Marekani, wakati wakiingia kwenye mji mkuu wa Kabul Agosti 5 baada ya kuchukua udhibiti wa maeneo mengine ya nchini hapo awali .

Msemaji wa Taliban Jumapili amesema kwamba Jumatatu itakuwa siku kuu ya kusherehekea mwaka mmoja wa ushindi dhidi ya Marekani na washirika wake. Vikosi vya kigeni vilivyokuwa vikiongozwa na Marekani viliondoka Afghanistan mwaka jana baada ya kuwepo chini humo kwa karibu miaka 20.

Utawala wa Taliban umekubali kutoruhusu taifa hilo kutumiwa na makundi ya kigaidi kama vile al Qaida, kufanya mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake. Utawala huo pia umeahidi kuheshimu haki za watu wa Afghanistan wakiwemo wanawake, bila kurejesha sera kandamizi zilizotumiwa na serikali kati ya 1996 na 2001.

XS
SM
MD
LG