Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 12:11

Maafisa wa Afghanistan wawashambulia wanawake waliokuwa wakidai haki zao


Mwanamke raia wa Afghanistan
Mwanamke raia wa Afghanistan

Vikosi vya usalama mjini Kabul, nchini Afghanistan, Jumamosi vilifyatua risasi hewani na kuwapiga wanawake waliokuwa wakipinga utawala wa Taliban leo huku wengi wao wakidai haki ya elimu, kazi na ushiriki wa kisiasa.

Vikosi vya usalama mjini Kabul, nchini Afghanistan, Jumamosi vilifyatua risasi hewani na kuwapiga wanawake waliokuwa wakipinga utawala wa Taliban leo huku wengi wao wakidai haki ya elimu, kazi na ushiriki wa kisiasa.

Hayo yalijiri katika mkesha wa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kundi hilo la Kiislamu kuchukua udhibiti wa nchi hiyo.

Walioshiriki kwenye mkutano wa hadhara waliimba "tunataka kazi, mkate, na uhuru" walipokuwa wakiandamana kuelekea Wizara ya Elimu katika mji mkuu wa Afghanistan kabla ya vikosi vya Taliban kujibu kwakutumia nguvu

Baadhi ya waandamanaji wanawake waliokimbilia katika maduka ya karibu walifukuzwa na kupigwa na vikosi vya usalama. Maafisa wa Taliban hawakuzungumza mara moja kuhusu madai hayo.

Kundi la Taliban lilitwaa udhibiti wa Afghanistan Agosti 15 mwaka jana kutoka kwa serikali ya Afghanistan inayoungwa mkono na kimataifa huku washirika wakiongozwa na Marekani na NATO wakiondoa wanajeshi wao nchini humo baada ya takriban miaka 20 ya vita na Taliban.

Serikali ya mpito ya wanaume wote wa kundi hilo la watu wenye misimamo mikali huko Kabul tangu wakati huo imerejesha nyuma, kwa kiasi kikubwa, haki za wanawake kufanya kazi, kupata elimu, na kuwazuia wasichana wengi wachanga, kurejea shule za sekondari, huku ikikiuka ahadi za Taliban za kuheshimu haki za Waafghanistan wote.

XS
SM
MD
LG