Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 04:58

Walinzi wa Iran wakabiliana na Taliban mpakani


Wanajeshi kutoka kikosi cha Taliban
Wanajeshi kutoka kikosi cha Taliban

Walinzi wa mpakani wa Iran Jumapili wamekabiliana na wale wa Taliban kutoka Afghanistan yakiwa makabiliano ya kwanza ya aina hiyo yangu Taliban kuchukua uongozi wa Afghanistan mwaka mmoja uliopita.

Radio ya Iran inayomilikiwa na serikali ya IRNA imemnukuu Meisam Barazandeh ambaye ni gavana wa jimbo la Hirmand mashariki mwa Iran, akidhibitisha tukio hilo, na kusema kwamba uchunguzi unaendelea, bila kutoa maelezo zaidi.

Upande wa Taliban haujatoa tamko kufikia sasa. Chombo cha habari cha Tasnim ambacho kinasemekana kuwa karibu na jeshi la Iran kimesema kwamba Taliban walianza kupiga risasi nyumba zilizoko upande wa Iran, wakati pia wakijaribu kupanda bendera kwenye eneo linalosemekana kuwa la Iran.

Makabiliano hayo yanaripotiwa kuchukua takriban muda wa saa moja kabla ya kumalizika Jumapili adhuhuri.

XS
SM
MD
LG