Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:38

Afghanistan yatangaza Jumatano kuwa siku kuu ya uhuru


Msichana akipeperusha bendera ya Afghanistan Jumatano wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja baada ya kuondoka kwa vikosi vya kigeni.
Msichana akipeperusha bendera ya Afghanistan Jumatano wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja baada ya kuondoka kwa vikosi vya kigeni.

Utawala wa Taliban  nchini Afghanistan Jumatano umetangaza siku kuu  ya kitaifa wakati  mji mkuu Kabul ukipambwa  kwa taa zenye kupendeza, ili kusheherekea mwaka mmoja baada ya kuondoka kwa vikosi vilivyoongozwa na  Marekani nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, viongozi wa taifa hilo wameweka sheria kali za kiislamu ambazo hazitambuliwi kimataifa na ambazo zimewatenga wanawake kwenye maisha ya kawaida.

Licha ya sheria hizo kali, pamoja na janga la kibinadamu linaloendelea kuongezeka, wakazi wengi wa Afghanistan wanasema kwamba wana furaha kwa kuwa vikosi vya kigeni vilivyochochea uasi wa Taliban hatimaye viliondoka baada ya vita vibaya vilivyodumu kwa miaka 20.

Msemaji wa serikali Zabihullah Mujahid kupitia ujumbe wa twitter amesema kwamba ni Siku kuu ya Uhuru, wakati mamlaka zikifanya sherehe rasmi kwenye kituo cha jeshi la anga cha Bagram, ambacho kilitumiwa na vikosi wa Marekani kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya Taliban.

XS
SM
MD
LG