Serhiy Popko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji wa Kyiv, aliandika kwenye mtandao wa Telegram kwamba shambulio hilo lilihusisha "idadi kubwa zaidi ya makombora katika muda mfupi zaidi."
Kikosi cha anga cha Ukraine kilisema kilidungua idadi isiyojulikana ya ndege zisizo na rubani na makombora yote 18, ambayo Russia ilirusha huko Kyiv, yakiwemo makombora 6 ya aina ya Kin-zhal.
Popko alisema shambulio hilo la angani ni la nane kulenga Kyiv tangu mwanzoni mwa mwezi huu.
Meya wa Kyiv Vitali Klish-ko alisema vifusi vilivyoanguka kutoka juu, vilisababisha uharibifu katika mitaa kadhaa ya mji mkuu, ikiwa ni pamoja na wilaya ya Solomya-nskyi ambapo watu watatu walijeruhiwa.
Uingereza ilisema Jumatatu kuwa inatuma mamia ya makombora zaidi ya Ukraine na ndege zisizo na rubani kwa matumaini ya kuimarisha uwezo wa kivita wa Ukraine, dhidi ya uvamizi wa Russia.