Umoja wa Mataifa mapema mwaka huu ulipiga kura ya kuunga mkono maadhimisho ya kile ambacho Wapalestina wanakitaja kama “al-Nakba” kwa Kiarabu, ambayo inatafsiriwa kama “janga.”
Waisraeli walipinga, hasa kwa Umoja wa Mataifa kupitisha neno Nakba, ambalo walisema linaunga mkono kikamilifu maoni kwamba kuundwa kwa nchi yao lilikuwa tukio la maafa.
Katika taarifa yake Jumatatu, Rosemary DiCarlo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kisiasa na kujenga amani alisema, wapalestina wanastahili maisha ya haki na utu na kutekelezwa kwa haki yao ya kujitawala na kujitegemea.