Zelenskyy atakuwa na mkutano na wanahabari akiwa pamoja na Waziri Mkuu Pedro Sanchez ambapo viongozi hao huenda wakatangaza mipango ya Uhispania kupelekea makombora ya Patriot na vifaru ya Leopard kwa Ukraine kama sehemu ya msaada wa dola bilioni 1.23 uliotangazwa mwezi uliopita, gazeti la El Pais limeripoti Jumatatu.
Zelenskyy atakuwa na mkutano na mfalme baada ya mkutano wake na Sanchez, ofisi ya ufalme imesema.
Zeleneskyy alitarajiwa kuitembelea Uhispania Mei 17 lakini safari iliakhirishwa, pamoja na safari nyingine za nje, huku kukiwa na mashambulizi ya Russia upande wa kaskazini katika mkoa wa Kharkiv.