Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameiahidi Kyiv msaada usio na masharti wa Marekani wakati wa ziara yake Jumanne mjini Kyiv. “Tuko pamoja nanyi leo. Na tutasimama na nyinyi hadi usalama wa Ukraine, uhuru, na uwezo wake wa kuchagua njia yake mwenyewe, umehakikishiwa”, Blinken alisema kulingana na shirika la habari la Reuters.
Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameishukuru Marekani kwa kile alichokiita “msaada muhimu”, alisema hayo wakati alipokuwa mwenyeji wa mazungumzo na Blinken. Bunge liliidhinisha na Rais wa Marekani Joe Biden alitia saini mwezi uliopita msaada wa dola bilioni 61 kwa Ukraine.
Msaada wa kijeshi kutoka Washington utaleta tofauti ya kweli dhidi ya uchokozi unaoendelea wa Russia kwenye uwanja wa vita, Blinken alimwambia Zelenskyy.
Forum