Rais wa Ukraine afurahishwa na msaada wa kijeshi kutoka Sweden

  • VOA News

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza katika Mkutano wa Usalama wa Munich in Munich, Ujerumani, Feb. 17, 2024.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Jumanne amefurahishwa na  msaada wa kijeshi wa dola za Marekani milioni 683 kutoka Sweden, ambao umekuja wakati viongozi wa Ukraine wakiendelea kushinikiza kupatiwa msaada zaidi wa kimataifa katika mapambano yao dhidi ya  uvamizi kamili wa Russia.

Zelenskyy ameuita msaada wa Sweden kuwa ni mchango muhimu kwa ajili ya Ukraine kujiimarisha wakati ambapo inakabiliwa na uchokozi wa Russia na uwekezaji wenye nguvu katika kudumisha amani na uhuru huko Ulaya.

“Risasi za mizinga, ulinzi wa anga, mfumo wa kurushia magruneti, boti za kivita, magari ya kivita, na vitu vingine vinakidhi baadhi ya mahitaji muhimu ya wapiganaji wetu walioko mstari wa mbele,” Zelenskyy alibandika ujumbe huu katika mitandao ya kijamii.

Waziri wa Ulinzi wa Sweden Pal Jonson alisema msaada ulikuwa mkubwa kabisa kuwahi kutolewa na nchi yake kwa Ukraine, na kwamba vifaa na silaha zinakidhi “baadhi ya mahitaji muhimu zaidi ya Ukraine.”

Pal Jonson

“Ukraine siyo tu kwamba inalinda uhuru wake lakini ni wa Ulaya yote,” Jonson alisema. “Sweden itasimama pamoja na Ukraine kwa kipindi chote itakachohitajika kufanya hivyo. Russia haiwezi kuruhusiwa kushinda vita hivi

Waziri Mkuu wa Ukraine Shmyhal alisema Jumanne kuwa wakati jeshi la Ukraine limepatiwa msaada na Marekani na Umoja wa Ulaya, inahitaji makombora ya masafa marefu kuimarisha mifumo yake ya ulinzi wa anga dhidi ya mashambulizi ya Russia.

“Kwa bahati mbaya, hivi sasa wana uwezo zaidi wa silaha za anga na inasikitisha kuwa hili limepelekea kuwepo maafa katika mstari wa mbele wa mapambano,” Shmyhal alisema.

Zelenskyy alisema Jumatatu baada ya kuzuru mstari wa mbele karibu na mji wa kaskazini mashariki wa Kupiansk kuwa Russia inatumia fursa ya kuchelewa kwa misaada ya kijeshi kwenda Ukraine.

“Hivi sasa kuna hali ngumu sana katika maeneo kadhaa ya mstari wa mbele, hasa kule ambako majeshi ya Russia yapo na wapiganaji wao wote wa akiba,” Zelenskyy alisema.

Msambazaji mkubwa kabisa wa msaada wa kijeshi wa Ukaine, ambaye ni Marekani, haijapeleka duru mpya ya misaada tangu mwezi Desemba wakati fedha zilipomalizika.

Rais wa Marekani Joe Biden amejitahidi kusukuma msaada wa dola bilioni 95 wa usalama wa kimataifa kwa ajili ya Ukraine, Israel and Taiwan kupitia Bunge la Marekani ambao unapingwa na wabunge kadhaa wa chama cha Republikan.

President Joe Biden returns to the White House, after a weekend in Delaware

Biden alisema Jumatatu atakuwa tayari kukutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson kujadili suala hilo.

“Bila shaka nitakuwa na furaha kukutana naye, iwapo ana chochote cha kuniambia,” Biden aliwaambia waandishi Jumatatu.

Wakati huo huo, Biden aligusia kuhusu wabunge wa Republikan kukataa kuendelea na ufadhili wa vita vya miaka miwili vya Ukraine wakijitetea dhidi ya uvamizi wa Russia.

“Jinsi wanavyoondoka kutoka katika vitisho vya Russia. Vile wanavyokaa mbali na NATO. Vile wanavyokaa mbali na kutekeleza majukumu yao … sijawah

Msemaji wa Johnson alisema spika alikuwa anajaribu kukutana na Biden kwa wiki kadhaa.

Raj Shah alimpongeza Biden “kwa kuwa tayari kukutana na Spika Johnson kuhusu njia bora kabisa ya kusonga mbele katika kulilinda taifa,” na kusema, “hatua hiyo imechelewa sana.”

Kwa kuungwa mkono na pande zote mbili, Baraza la Seneti linalodhibitiwa na Wademokrat liliidhinisha msaada huo wa matumizi.

Johnson, kiongozi wa Warepublikan walio na wingi mdogo katika Baraza la Wawakilishi, anasita kulipeleka suala hilo katika ukumbi wa Baraza hilo ili lipigiwe kura, kwa upande fulani kwa sababu Rais wa zamani Donald Trump anapinga msaada huo mpya.

Johnson amelalamika kuwa msaada huo wa nje hauna udhibiti mpya wa kuzuia kuingia kwa maelfu ya wahamiaji haramu wanaovuka mpaka kutoka Mexico kuja Marekani.

Lakini Warepublikan katika Baraza la Seneti, kwa ombi la Trump, walizuia wazo la pendekezo la vyama vyote viwili kuimarisha udhibiti uhamiaji.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AFP, AP, na Reuters.