Rais wa Indonesia autahadharisha umoja wa Asean kuonekana kutokuwa na umuhimu

Rais wa Indonesia Joko Widodo

Rais wa Indonesia Joko Widodo Jumatano ametoa wito kwa  umoja miongoni mwa mataifa ya Asia kusini mashariki (ASEAN), wakati shinikizo likiongezeka la  kumaliza ghasia zinazoikumba Myanmar au jumuiya hiyo kujihatarisha kuonekana kutokuwa na umuhimu.

Machafuko nchini Myanmar inayoongozwa na serikali ya mpito yametawala mazungumzo katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa ya Asia kusini mashariki nchini Indonesia.

Wakati huo huo jumuiya hiyo ya kikanda imekuwa ikikosolewa kwa kutochukua hatua.

Hata hivyo ASEAN imeongoza majaribio ya kidiplomasia kutatua mzozo lakini juhudi zake hadi sasa zimeshindwa kukomesha umwagaji damu uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021.

Jeshi hilo limeepuka ukosoaji wa kimataifa na kukataa kushirikiana na wapinzani wake ambao ni pamoja na wabunge walioondolewa madarakani, makundi yanayopinga mapinduzi , makundi ya makabila madogo yenye silaha.