Muungano huo unaonekana kuendelea kushamiri wakati mataifa mengine kama Marekani yakishirikiana na muungano huo katika kudhibiti ushawishi wa China kwenye eneo la Indo Pacific. Kuanzia Alhamisi, New Delhi itakuwa mwenyeji wa kikao cha siku mbili cha mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya ASEAN, yakiwa maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano wao wakati wakizungumzia ushirikiano zaidi.
Mwaka huu wa 2022 umetengwa kama mwaka wa urafiki wa India na ESEAN. Mataifa wanachama wa ASEAN ni pamoja na Singapore, Thailand, Vietnum, Brunei, Cambodia, Indonesia, Laos. Malaysia, Myanmar na Ufilipino.