Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:15

Wanadiplomasia wa ASEAN wakubaliana kushughulikia masuala muhimu


Wanadiplomasia wa nchi za kusini mashariki mwa Asia waliokutana Cambodia katika mkutano wa ASEAN
Wanadiplomasia wa nchi za kusini mashariki mwa Asia waliokutana Cambodia katika mkutano wa ASEAN

Wanadiplomasia wa juu wa kusini mashariki mwa Asia wanaokutana katika mji mkuu wa Cambodia wameongeza juhudi za kusimamisha kusambaa kwa ghasia nchini Myanmar.

Katika mkutano wapo pia wameadhimia kushughulikia masuala mangine muhimu ambayo mara kwa mara yana mgawanyiko wa kikanda.

Huu ni mkutano wa kwanza unaowakutanisha mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya mataifa ya kusini mwa Asia na kuhudhuriwa moja kwa moja toka kuzuka kwa janga la Covid-19, ambalo limedhoofisha uchumi na kusumbua diplomasia.

Mkutano unafanyika hivi sasa wakati kuna ongezeko la wasi wasi baina ya Marekani na China pamoja na kuongezeka tatizo la la upungufu wa chakula duniani, na kupanda kwa bei ya nishati baada ya Russia kuivamia Ukraine.

XS
SM
MD
LG