Ramaphosa akanusha njama za kisiasa kusababisha kurudi kwa umeme Afrika Kusini

Rais na kiongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia umati katika Kongamano la Muungano wa Wafanyakazi wa Afrika Kusini Mai 1, 2024. Picha na RODGER BOSCH / AFP.

Rais Cyril Pamaphosa wa Africa ya kusini amekanusha madai ya upinzani kwamba kusitishwa hivi karibuni ugavi wa umeme  inatokana na uchaguzi ujao wa mai 29.

Chama kikuu cha upinzani Democratik alliance wiki iliyopita ilidai kwamba kuimarika kwa huduma za umeme kunatokana na uingiliaji wa kisiasa uliofanywa na ANC. Kinakituhumu chama hicho tawala kwa kuiwekea shinikizo kampuni ya umemke ya Eskom kuhakikisha umeme unapatikana.

Katika kipindi cha mwaka jana kiwango cha ugavi wa umeme kilifikia kilele chake na kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka huu. Lakini tangu kipindi cha kampeni huduma zimerudi kuwa sawa.

Ramaphosa amesema kwamba Kuimarika kwa huduma za Eskom inaonesha kwamba mpango wa nishati wa serikali ulotangazwa 2022 unafanya kazi na unazaa matunda.