Rais Cyril Ramaphosa leo Jumamosi amejigamba kuhusu mafanikio ya Afrika Kusini chini ya uongozi wa chama chake wakati nchi hiyo inasherehekea miaka 30 ya demokrasia, mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wake utakaokuwa na matokeo makubwa katika miongo kadhaa.
Raia wa Afrika Kusini wanapiga kura Mei 29, miongo mitatu baada ya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 1994, uliomaliza utawala wa wazungu na kumfanya Nelson Mandela na chama cha African National Congress (ANC) kuingia madarakani.
“Afrika Kusini leo ni mahali pazuri zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 30 iliyopita,” Ramaphosa alisema katika hotuba yake ya kuadhimisha Siku ya Uhuru kwenye Majengo ya Muungano, ambako ni makao makuu ya serikali, mjini Pretoria.
Kiongozi huyo mwenye miaka 71 alitumia fursa hiyo sherehe hizo kuorodhesha maboresho yaliyofanywa na chama cha ANC, ambacho hakifanyi vizuri katika kura za maoni, na kiko hatarini kupoteza wingi wake wa viti bungeni kwa mara ya kwanza.
Forum