Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na familia yake ni miongoni mwa viongozi wa dunia wanaosemekana kuwa wameficha mabilioni ya dola katika akaunti za siri nje ya nchi.
Rekodi ilizopata jumuiya ya kimataifa ya wanahabari wa uchunguzi, zinaonyesha kwamba familia ya Kenyatta ina utajiri wa dola nusu bilioni, uliohusishwa katika angalau taasisi saba na katika nchi mbali mbali.
Fedha hizo zinadaiwa kuwekwa nchi ambazo hazitozwi kodi ikiwemo Panama, British Virgin Islands.
Familia iliorodhesha huduma ya moja ya mabenki makubwa zaidi nchini Uswisi, Union Bancaire Privee, kusajili na kuanzisha taasisi huko Panama, ili kusimamia na kuangalia utajiri wake ambao ulianza kujengwa chini ya enzi ya Jomo Kenyatta.
Jomo Kenyatta alikuwa rais wa kwanza wa Kenya, mnamo mwaka 1964 baada ya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza.