Rais Biden kufanya mkutano wa kwanza na waandishi

Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza kutoka ikulu juu ya mauaji ya Colorado, March 23, 2021.

Rais wa Marekani  Joe Biden anatarajiwa kukutana na  waandishi wa habari Alhamisi huko ikulu ya Marekani katika  mkutano wake wa kwanza na wanahabari  tangu aingie madarakani mwezi Januari.

Wakati Biden amerudisha tena mikutano ya kila siku ya msemaji wake na waandishi wa habari na kujibu maswali katika muundo mwingine wa habari , yeye ndiye rais wa kwanza katika miongo minne kuchukua muda huo katika muhula wake wa kwanza bila kufanya kikao rasmi cha maswali na majibu na waandishi wa habari.

Ni fursa kwake kuzungumza na Wamarekani, kwa hakika moja kwa moja kupitia wana habari, msemaji wa ikulu Jen Psaki aliwaambia waandishi wa habari Jumanne. Kwa hivyo nadhani anafikiria juu ya kile anachotaka kusema, kile anataka kuwasilisha, ni wapi anaweza kutoa taarifa mpya anatazamia fursa ya kushirikiana na vyombo vya habari huru alisema Psaki.

Biden huenda akakabiliwa na maswali juu ya mada kadhaa zenye mvutano za ndani, ikiwa ni pamoja na upigaji risasi wa watu wengi huko Georgia na Colorado, hali katika mpaka wa Marekani na Mexico na majibu ya serikali kuhusiana na janga la corona.