Rais Abbas wa Palestina anakabiliwa na upinzani kwa mara ya kwanza

Rais wa Palestinat Mahmoud Abbas

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 15 Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas anakabiliwa na upinzani katika uchaguzi, huku mpasuko ndani ya chama chake chenye nguvu cha Fatah unaleta tishio jipya la utawala wake juu ya siasa za Wapalestina.

Kulingana na shirika la habari la Uingereza, Reuters, juhudi za kujitenga kwa mmoja wa washirika katika chama cha Abbas zimeongeza uvumi kuwa huenda akafuta upigaji kura wa rais uliopangwa kufanyika mwezi Julai,

Sababu zinazo elezwa ni Abbas anahofia changamoto kutoka kwa Marwan Barghouti, kiongozi maarufu wa Wapalestina ambaye ametiwa gerezani na Israel.

Wapalestina wakiandamana kupinga kushikiliwa kwa kiongozi wa Palestina Marwan Barghouti wakionyesha mshikamano na Wapalestina wanashikiliwa na serikali ya Israelii.

Ofisi ya Abbas imekanusha kuwa ana mipango ya kuchelewesha au kufuta uchaguzi wa rais.

Bargout mwenye umri wa miaka 61, amekuwa nii kiini katika upinzani wa wapalestina mwaka 2000 – 2005 katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza yanayo kaliwa kimabavu na Israel.

Alihukumiwa na mahakama ya Israel mwaka 2003 kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya mashambulizi kadhaa mabaya kwa Waisraeli yaliyofanywa na wanamgambo wa kipalestina.

Barghouti alikana mashtaka hayo. Abbas mwenye umri wa miaka 85, mwezi Januari alitangaza uchaguzi wa rais na wabunge hatua ambayo inaonekana kama majibu kwa ukosoaji wa ndani na magharibi juu ya uhalali wa kidemokrasia kwa urais wake.