Mwanzoni, maandamano ya amani yalianza mwezi uliopita dhidi ya msuada wa fedha uliolenga kuongeza kodi, lakini yaligeuka na kuwa ghasia zilizopelekea vifo vya watu wa kadhaa.
Ruto alitupilia mbali msuada huo na badala yake kuomba kuwa na mjadala wa kitaifa. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Raila amesema kuwa,”Haki lazima iwepo kabla ya mazungumzo yoyote.” Licha ya pendekezo hilo, maandamano yameendelea kote nchini, wakati upinzani ukiitisha maandamano mapya wiki ijayo.
Uamuzi wa mahakama wa Alhamisi uliondoa marufuku ya polisi ya kuzuia maandamano kwenye mji mkuu. Ruto kwa upande wake ameonya wale ameita wezi na wauaji, wanaohatarisha usalama wa taifa. Ameongeza kusema kuwa “tunataka nchi yenye amani, ambapo masuala yanasuluhishwa kwa njia ya kidemokrasia.
Ijumaa Ruto alitangaza sehemu ya orodha ya mawaziri wapya wa baraza lake, likini upinzani mara moja ulikosoa chaguo lake, huku pia ukisema uwa hautaunda serikali ya muungano naye.