Kuachiwa kwa mateka hao ni kwa mabadilishano ya sitisho rasmi la mapigano kwa siku tatu, afisa mmoja anayetoa taarifa kuhusiana na mazungumzo hayo aliliambia shirika la habari la Reuters.
Mpango huo, unaojadiliwa, ambao umeratibiwa na Marekani, pia unatazamia kuiona Israel ikiwaachilia baadhi ya wanawake wa Kipalestina na watoto kutoka jela za Israel na kuongeza kiwango cha misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia Gaza, afisa huyo alisema.
Itaweka alama ya kuachiliwa kwa idadi kubwa ya mateka waliokuwa wakishikiliwa na Hamas tangu kundi la wanamgambo wa Wakipalestina kuvuka mpaka wa Gaza, kushambulia sehemu za Israeli na kuwachukua mateka katika eneo hilo.
Hamas wamekubaliana na jumla ya muhtasari wa mpango huu, lakini Israel haijafanya hivyo na bado inashauriana kuhusu maelezo na mpango huo, alisema afisa huyo.
Haijulikani ni wanawake na watoto wangapi wa Kipalestina, Israeli itawaachia kutoka jela zake kama sehemu ya makubaliano chini ya majadiliano hayo.
Nchi hiyo tajiri ya Ghuba ya Qatar, ambayo ina utashi na malengo ya sera za mambo ya nje, ina mawasiliano ya moja kwa moja na Hamas pamoja na Israeli. Hapo awali ilisaidia kuwapatanisha wawili hao.
Makubaliano kama hayo yanaitaka Hamas kukabidhi orodha kamili ya mateka waliosalia huko Gaza.
Mpango wa kuwaachilia mateka wote sasa hivi haujadiliwi, afisa huyo alisema.
Hakuna majibu ya haraka kutoka kwa maafisa wa Israel, ambao hapo awali walikataa kutoa maoni ya kina kuhusu mazungumzo ya mateka, akitoa mfano wa kusita kudhoofisha diplomasia au ripoti za uchochezi inazoziona kama "vita vya kisaikolojia" vinavyofanywa na wanamgambo wa Kipalestina.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters