Putin amesema ndege za kivita za F-16 huenda zikafanya aina fulani ya mashambulizi dhidi ya majeshi ya Kremlin kwa kutumia vituo hivyo, akisema vituo hivyo huenda vikawa “lengo halali.”
F-16 zinahitaji njia maalum za ndege na kuimarisha jengo la kuhifadhi ndege ili kuzilinda wakati zikiwa ardhini.
Wachambuzi wa kijeshi wamesema kuwasili kwa dazeni ya ndege za F-16 huenda ikabadili hali, ingawaje maafisa wa Ukraine wamekaribisha fursa hiyo ya kujibu utawala wa Russia katika anga.
Hata hivyo, Putin amesema Russia haina azma ya kuanzisha vita na NATO.
Amesema ni “ujinga mtupu” kufikiria kwamba Russia huenda ikamshambulia nchi mwanachama wa NATO.