Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:26

Russia yasema mashambulizi ya roketi yamedhibitiwa, Ukraine yaeleza imeshambuliwa usiku kucha


(From left to right) Russian President Vladimir Putin, Ukrainian President Volodymyr Zelenskyy and U.S. President Joe Biden.
(From left to right) Russian President Vladimir Putin, Ukrainian President Volodymyr Zelenskyy and U.S. President Joe Biden.

Russia ilisema Jumatano imezuia mashambulizi ya roketi yaliofanywa na Ukraine yakiulenga mkoa wa Belgorod, wakati Ukraine ilisema Russia imeishambulia usiku kucha kwa droni 13.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema mfumo wa ulinzi wa anga wa nchi hiyo umetungua roketi 18 zilizorushwa na Ukraine.

Vyacheslav Gladkov, gavana wa Belgorod, alisema kupitia mtandao wa Telegram kulikuwa na uharibifu kidogo wa majumba katika vijiji kadhaa, na mtu asiyepungua mmoja alijeruhiwa.

Belgorod, iliyoko katika eneo la mpakani kati ya Russia na Ukraine, inalengwa mara kwa mara katika mashambulizi dhidi ya Ukraine wakati nchi hiyo ikitafuta njia ya kutokomeza uvamizi wa Russia ulioanza zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Jeshi la Ukraine lilisema limetungua droni 10 kati ya 13 za Russia, huku zikizuia mashambulizi katika mikoa ya Kharkiv, Sumy na Kyiv.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alitangaza jioni Jumanne mabadiliko ya timu yake ya usalama wa taifa.

Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila siku usiku kuwa Oleksiy Danilov, katibu wa baraza la usalama wa taifa la Ukraine, nafasi yake imechukuliwa na Oleksandr Lytvynenko, ambaye kabla aliongoza shirika la ujasusi wa nje la Ukraine.

Zelenskyy aliyaita mbadiliko hayo kuwa ni sehemu ya “kuimarisha mfumo wa utawala wa taifa letu.”

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG