Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:02

Ukraine yatungua makombora 31 ya Russia


Jeshi la anga la Ukraine, linasema limetungua makombora 31 yaliyo husishwa katika mashambulizi ya anga ya Russia yaliyolenga mji mkuu wa Ukraine, Kyiv,  Alhamisi.

Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko, amesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba mabaki ya roketi yaliangukia sehemu za wilaya kadhaa za mji katika majumba wanayoishi wakazi na kusababisha moto.

Meya Klitschko amesema takriban watu 10 walijeruhiwa katika matukio hayo. Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, akitumia mitandao ya kijamii leo hii amesema kwamba matukio kama hayo ya kutisha hutokea usiku na mchana.

Rais huyo ameendelea kutoa mwito wa msaada kutoka kwa washirika wa Ukraine, hasa kupatiwa mifumo ya ulinzi wa anga.

Mashambulizi hayo ya Kyiv, yamefanyika siku moja bada ya rais Zelenskyy, kuwa mwenyeji wa mshauri wa usalama wa taifa wa White House, Jake Sullivan kwa mazungumzo.

Forum

XS
SM
MD
LG